HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa wauguzi uliodumu zaidi ya siku 150 wafikia kikomo

Wauguzi waliokuwa mgomo wameagizwa kurejea kazini kuanzia ijumaa. Hii ni baada ya kuwepo makubaliano baina ya serikali kuu na zile za kaunti kuhusiana na lalama zao. Waziri wa afya Dkt Cleopa Mailu ameahidi mkataba baina yao na wauguzi utatekelezwa pindi utakaposainiwa ili ni mgomo ambao umedumu kwa zaidi ya siku 150, na kuathiri huduma za afya katika serikali za kaunti. Na baada ya mkutano na washika dau katika sekta ya afya, maafikiano hayo yamepeleka wauguzi kupata nyongeza ya marupupu ya huduma za uuguzi na ile ya sare zao. Wamekubaliana pia mishahara yote ya wauguzi ya kuanzia mwezi Septemba italipwa na hakuna atakayechukuliwa hatua kwa kushirki mgomo.

Show More

Related Articles