HabariMilele FmSwahili

Wateja wa NHIF kupokea huduma za kiafya kutoka hospitali yoyote illiyo na idhini ya hazina hiyo

Wateja wa NHIF sasa wataweza kupokea huduma za kiafya kutoka hospitali yoyote iliyona idhini ya hazina hiyo. Afisa mkuu mtendaji wa NHIF Geofrey Mwangi anasema wameondoa sharti ya mteja kuhudumiwa kutoka orodha aliyochagua. Mwangi anasema kila mteja ana idhini ya kutumia hospitali anayotaka japo sio zaidi ya mara nne kwa mwaka. NHIF ambayo inazaidi ya wateja milioni 24 inalenga kuwavutia wakenya zaidi kujiunga na hazina hiyo kujifaidi kwenye gharama ya tiba

Show More

Related Articles