HabariMilele FmSwahili

Mkongwe wa miaka 95 ajitia kitanzi Kyuso, Kitui

Polisi katika eneo la Kyuso kaunti ya Kitui wanachunguza kisa cha mkongwe wa miaka 95 kupatikana kujitia kitanzi kwenye paa la chumba chake, baada ya kwenda kulala jana jioni. Kamanda wa AP kaunti ya Kitui Benson Wasike, amedhibitisha kupokea maelezo kutoka kwa mwanae aliyempata zakayo mwinza. Kulingana na Wasike mwili wa mwenda zake haukuwa na majeraha yeyote ila uvimbe shingoni, na hawakupata ushahidi wowote wa njama yake kujiua.

Show More

Related Articles