HabariMilele FmSwahili

Mahakama kuu yatupilia mbali ombi la kubatilisha ushindi wa Benjamin Washiali

Mahakama kuu imetupilia mbali ombi la kubatilisha ushindi wa mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali. Mahakama hiyo imechukua hatua hiyo kwa misingi kuwa hati ya kiapo cha kesi dhidi ya washiali iliwekwa sahihi na mawakili bandia. Washiali ambaye pia ni kiranja wa wengi bungeni aliwasilisha kesi mahakamani kutaka ombi la mlalamishi David Wamatsi kutupwa kwa madai hati yake ya kiapo iliandaliwa kinyume na sheria

Show More

Related Articles