HabariMilele FmSwahili

Wahadhiri wa vyuo vikuu kuendelea na maandamano yao leo

Wahadhiri kutoka vyuo vikuu 28 vya umma wanaendelea na maandamano yao leo kushinikiza kutekeleza kwa matakwa yao. Wahadhiri hao chini ya mwavulu wa UASU wanataka mkataba waliotia saini kuruhusu nyongeza ya mishahara na marupurupu ya nyumba kuanza kutekelezwa mara moja. Katibu Constatine Wasonga ameilamu serikali akisema imekuwa ikiwahadaa na kushikilia hawatarejea kazini hadi shilingi bilioni 5.2 za kufanikisha mkataba huo zitakapotolewa

Show More

Related Articles