HabariMilele FmSwahili

Askari 7 wa jiji la Nairobi wafikishwa mahakamani kwa kosa la wizi wa kimabavu

Askari 7 wa jiji la Nairobi wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na kosa la wizi wa  kimabavu. Askari hao akiwemo Philemon Cheburet Kimei, Peter Ndungu Gitau na Bernard Maina Kogi wanadaiwa kumuibia Cyrus Ndumia  shilingi 600 wakiwa wamejihami kwa siala butu. 7 hao wamefikishwa mbele ya hakimu mkuu Peter Miriam Mugure. Wanne kati yao wameachiliwa kwa thamana ya shilingi 100,000 huku kesi hiyo ikitarajiwa kusikizwa tarehe 30 mwezi huu wa novemba.

Show More

Related Articles