HabariMilele FmSwahili

Nyumba zaidi ya 20 zateketea katika mkasa wa moto Nyeri

Zaidi ya nyumba 20 zimeteketea kufuatia mkasa wa moto katika mtaa wa chania mjini Nyeri. Kulingana na mmiliki nyumba hizo Jared Githaiga  familia zaidi ya 20 zimeathirika. Aidha mkasa huo umewaacha wakazi kwa mahangaiko wakilalamikia kutoweza kuokoa chochote. Upepo mkali na nyumba katika eneo hilo kujengwa kwa mbao kumeripotiwa kuchangia moto huo kusambaa kwa haraka. Chanzo cha mkasa huo hakijabainika. Naibu kamishna kaunti ya Nyeri John Marete amedhibitisha kuwa hakuna aliyejeruhiwa na kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto huo.

Show More

Related Articles