HabariMilele FmSwahili

Kenya yaorodheshwa ya themanini katika mataifa yaliyo na mazingira bora ya kibiashara

Kenya imepanda kutoka nambari 92 hadi 80 katika orodha ya mataifa yaliyo na mazingira bora ya kufanyia biashara. Ripoti kutoka Benki ya dunia inaonyesha nguzo 6 ambazo Kenya imewezesha mazingira hayo ikiwemo umeme, muiundo msingi pamoja na sheria legevu. Wakielezea furaha yao kuhusu ripoti hiyo, waziri wa viwanda Adan Mohamed amewahakikishia wawekezaji wa humu nchini na wale kutoka nje kwamba serikali itaendelea kuwapa mazingira ya kufanyia kazi, wito uliotiliwa mkazo na afisa mkuu mtendaji wa muungano wa wafanyabiashara wa kibianfsi KEPSA, Carol Kariuki

Show More

Related Articles