HabariMilele FmSwahili

Viongozi wa jubilee waendelea kupinga wito wa Raila kuandaliwa uchaguzi mpya wa urais

Viongozi wa Jubilee wameendelea kupinga vikali wito wa kinara wa NASA Raila Odinga kuandaliwa uchaguzi mpya wa urais katika siku tisini. Gavana wa Nyeri Wahome Gakuru amepuuza madai ya Raila kuwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 haukuwa huru na wazi. Ametaja madai ya Raila kama ya kibinafsi na kumtaka kuheshimu uamuzi wa wakenya. Pia amemsuta Raila kwa madai ya kutaka kuzua machafuko nchini kwa kutangaza kubuni bunge la wananchi.

Show More

Related Articles