HabariMilele FmSwahili

Watu 8 wafariki baada ya kukogongwa na gari mjini Newyork Marekani

Watu nane wamefariki dunia na zaidi ya kumi na wawili kujeruhiwa baada ya gari kuwakanyaga waendesha basikeli mjini Newyork Marekani meya wa mji huo Bill De Blasio, ametaja tukio hilo kuwa ugaidi wa namna yake. Naye kamishna wa polisi wa jiji la New York, James O’Neill, amesema mtu aliyehusika kutekeleza tukio hilo ni kijana wa miaka ishirini na tisa aliyekuwa anaendesha gari dogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.

Show More

Related Articles