HabariMilele FmSwahili

NASA yadai ni wapiga kura milioni 2.5 pekee walioshiriki uchaguzi Oktoba 26

Muungano wa NASA sasa unadai ni wapiga kura milioni 2.5 pekee walishiriki uchaguzi wa Oktoba 26. Kupitia msemaji wa NASA Salim Lone wanadai vifaa vya KIEMS vinaonyesha wapiga kura milioni 2.5 pekee walipiga kura na wengine milion 5 walipatikana kwa njia ya mkato. Katika taraifa kwa vyombo vya habari, NASA imedai rais Uhuru Kenyatta hakupata ushindi kihalali na wanataka uchaguzi mpya baada ya siku 90. Aidha wamewapongeza waangalizi wa kimataifa waliokosa kuhudhuria hafla ya kutangazwa matokeo ya urais ukumbini Bomas wakisema hatua hiyo inaonyesha uhuru wao kuonyesha msimamo wao dhidi ya uchagizi huo.

Show More

Related Articles