HabariPilipili FmPilipili FM News

wakenya Wasubiri hatua ya Raila Kwa Hamu

Wakenya wanasubiri kwa hamu kusikia hatua ya kisiasa itakayochukuliwa na muungano wa upinzani NASA.

Kinara wa NASA Raila Odinga aliwaahidi wafuasi wake kwamba atawaelezea hatua wanazopania kuchukua baada ya kususia uchaguzi wa urais ulioandaliwa wiki jana.

Inasubiriwa kuona ni hatua gani Raila atachukua baada ya kusema hawatambui ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Tayari Raila ametangaza kubadili muungano wa NASA kuwa vuguvugu la upinzani.

Show More

Related Articles