Pilipili FmPilipili FM News

CIPK Yawashukuru Wakenya Kwa Kudumisha Amani Wakati Wa uchaguzi.

Baraza la Maimam na wahubiri nchini CIPK limewashukuru wakenya kwa kudumisha amani, wakati wa marudio ya uchaguzi, na kuwaomba kuendelea na moyo huo huo wakati huu taifa likisubiri kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta,na hata baada ya kuapishwa kwake.
Viongozi hao wa kidini, wakiongozwa na katibu mkuu wa baraza hilo Sheikh Mohammed Khalifa, wameomba wale walio shindwa kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki.

Show More

Related Articles