HabariMilele FmSwahili

Waangalizi wa uchaguzi wa AU wasifia uchaguzi uliompa Uhuru ushindi

Waangalizi wa uchaguzi kutoka muungano wa Afrika wamesifia uchaguzi wa urais uliompa ushindi rais Uhuru Kenyatta. Kundi hilo likiongozwa na aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki linasema maafisa wake walishuhudia zoezi zima la kuthibitisha fomu zilizowasilishwa katika ukumbi wa Bomas bila dosari zozote kushuhudiwa. Kwenye ripoti yake ya mwanzo ya uchaguzi uliokamilika Alhamisi, kundi hilo limelalamikia matukio ya ghasia haswa katika ngome za upinzani. Vilevile Mbeki na waangalizi wa AU wametoa wito kwa wasioridhishwa na matokeo ya uchaguzi kufika mahakamani.

Show More

Related Articles