HabariPilipili FmPilipili FM News

Bob Collymore Amechukua Likizo Ya Miezi Kadhaa Ili Kupokea Matibabu.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Safaricom Bob Collymore amechukua likizo ya miezi kadhaa ili kupokea matibabu.

Katika taarifa mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo,Nicholas Nganga anasema wadhifa wa Collymore sasa utashikilia kikaimu na Sateesh Kamath ambaye wakati huu anahudumu kama afisa mkuu wa mahesabu katika kampuni hiyo.

Nganga anasema sateesh atasaidia kwa karibu na Joseph Ogutu ambaye atasimamia majukumu ya kila siku ya kampuni hiyo hadi Collymore atakaporejea.

 

Show More

Related Articles