HabariPilipili FmPilipili FM News

Raila Kutangaza Mwelekeo Wake Wa Kisiasa.

Muungano wa NASA unatarajiwa kutangaza mwelekeo wake wa kisiasa hii leo.

Kinara wa NASA Raila Odinga aliwaahidi wafuasi wake kwamba atawaelezea hatua wanazopania kuchukua baada ya kususia uchaguzi wa urais ulioandaliwa wiki jana.

Inasubiriwa kuona ni hatua gani Raila atachukua baada ya kusema hawatambui ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Tayari Raila ametangaza kubadili muungano wa NASA kuwa vuguvugu la upinzani.

Show More

Related Articles