HabariMilele FmSwahili

Msafara wa waziri Matiangi wavamiwa na vijana mtaani Kawangware

Polisi wamekabiliana na makundi ya vijana walioanza kurusha mawe  katika shule ya msingi ya Gatina mtaani Kawangware hapa Nairobi wakati wa ziara ya waziri wa elimu Fred Matiangi katika shule hiyo. Vijana hao waliowashambulia wanahabari na wanafunzi kwa mawe walikuwa wakishinikiza kuhutubiwa na waziri matiangi. Waziri Matiangi alikuwa amezuru shule hiyo ya Gatina kutathmini maandalizi ya mtihani wa KCPE unaoanza rasmi hapo kesho. Ni kisa kilichotokea muda mfupi baada ya inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet kuwahakikishia wanafunzi hao usalama wao wakati wa mtihani.

Show More

Related Articles