HabariMilele FmSwahili

Marekani yaelezea hofu kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa nchini

Marekani imeelezea hofu kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo baada ya uchaguzi wa juma jana. Balozi wa Marekani nchini Michael Godec amewataka viongozi na wanasiasa kujitokeza wazi kushtumu machafuko hayo na kuhubiri amani. Wametaka kuchunguzwa kwa  polisi wanaodaiwa kuhusika na vifo vya watu waliouwawa kwa kupigwa risasi na wengine kujeruhiwa wakati wa  maandamano. Marekani imetaka kuandaliwa kwa  mazungumzo ya kitaifa yatakayoshirikisha kila mkenya ili kutafuta mwafaka kwa  hali iliyoshuhudiwa nchini.

Show More

Related Articles