HabariMilele FmSwahili

Watu 2 waangamia kutokana na mkurupuko wa kipindupindu Embu

Watu wawili wameangamia huku wengine 26 wakiwa mahututi katika hospitali kadhaa kaunti ya Embu kufuatia mkurupuko wa kipindupindu. Wawili hao wanaarifiwa kufariki wakati wakipokea matibabu katika hospitali za siakago na runyenjes level 4. Waziri wa afya katika serikali ya kaunti hiyo Dkt Jamlek Muturi amesema waathiriwa waliolazwa wametengwa katika wodi maalum ili kuzuia ugonjwa huo kusambaa. Muturi amesema kundi la madaktari limetumwa kuchunguza maji ya miti kubaini iwapo ina viini vya ugonjwa huo. Aidha uchuuzi wa vyakula na watu kula katika sherehe pia kumepigwa marufuku.

Show More

Related Articles