HabariMilele FmSwahili

Rais atuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha askofu Cornelius Korir

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kufuatia kuaga dunia kwa askofu Cornelius Korir. Rais amesema Korir atakumbukwa kwa kuhusika katika kudumisha amani kanda ya North Rift. Naye mwenyekiti wa baraza la magavana Josephat Nanok katika taarifa amesema askofu Korir atakumbukwa kwa juhudi zake katika kukabili tatizo la wizi wa mifugo na pia kuhubiri utangamano kufuatia machafuko ya kikabila katika eneo la Burnt Forest mwaka 1992 na baada ya uchaguzi wa 2008. Kauli sawa imetolewa na gavana na Elgeyo marakwet Alex Tolgos.

Show More

Related Articles