HabariMilele FmSwahili

Usalama waimarishwa katika ukumbi wa Bomas

Usalama umeimarishwa katika ukumbi wa Bomas tume ya IEBC ikikaribia kukamilisha shughuli ya kujumulisha matokeo ya uchaguzi wa urais. Maafisa wa usalama wanakagua vikali kila anayeingia katika ukumbi huo huku  magari yakizuiwa kuingia. Hayo yanajiri huku tume ya uchaguzi IEBC inatarajiwa kumtangaza leo mshindi wa uchaguzi wa marudio wa urais. Tayari  fomu zote 34B kutoka maeneo bunge 266 yaliyoshiriki uchaguzi kuwasili katika kituo cha Bomas. Aidha matokeo yaliyodhibitishwa na IEBC kwa mujibu wa fomu hizo yanamweka kifua mbele rais uhuru kenyatta kwa kura milioni 7.4 IEBC ikitarajiwa kumtangaza mshindi.

Show More

Related Articles