HabariK24 TvSwahiliVideos

Viongozi wa Jubilee wataka wachochezi kukabiliwa kisheria

Wakereketwa wa Jubilee wakiongozwa na aliyekuwa mbunge Ababu Namwamba sasa wanasema kinara wa NASA Raila Odinga atawajibikia ghasia ambazo huenda zikatokea baada ya kutangazwa matokeo ya urais.

Ababu ameleza wameandikia umoja wa bara Afrika A.U na muungano wa IGAD kuelezea mpango wa Raila kuchochea ghasia baada ya kususia uchaguzi wa Oktba 26.

Haya yanajiri wakati ambapo baadhi ya viongozi kutoka ukambani wakiitaka serikali kuchunguza vuguvugu la National Resistance Movement wakiwaomba wanajamii wakamba wasihusishwe na vuguvugu hilo.

Show More

Related Articles