HabariMilele FmSwahili

Wanyama: Ni maeneo chache yaliyoshuhudia ghasia kaunti ya Bungoma

Ni maeneo chache ya kaunti ya Bungoma yaliyoshuhudia ghasia za wafuasi wa NASA. Ndio usemi wa mbunge wa Webuye Magharibi Dan Wanyama anayesema kuwa vijana waliohusika kwenye vurugu za uchaguzi hapo jana zilizopelekea kuuwawa kwa mtu mmoja hawakuwa wenyeji wa kaunti ya Bungoma bali walisafirishwa kutoka nje. Anasema maeneo mengine ya kaunti yalisalia kuwa tulivu baada ya uchaguzi akielezea kuridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza kaunti ya Bungoma.

Show More

Related Articles