HabariMilele FmSwahili

IEBC yataka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mbunge Alice Wahome

Tume  ya IEBC inasema hatua za kisheria zinastahili kuchukuliwa dhidi ya mbunge wa kandara Alice Wahome kwa kumdhulumu afisa wa IEBC huko Muranga. Wahome alizozana na msimamizi wa uchaguzi kaunti ya Muranga Martin Malonza katika kituo kikuu cha kuhesabia kura katika shule ya Ng’araria na hata kumvuta afisa huyo akitaka kutia saini kwenye fomu ya 34B kama ajenti wa Jubilee. Katika ujumbe IEBC inasema huo ni ukiukaji wa sheria za uchaguzi.

Show More

Related Articles