HabariMilele FmSwahili

ELOG yaeleza kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyoandaliwa

Kundi la waangalizi wa uchaguzi ELOG limeelezea kuridhishwa na jinsi uchaguzi wa urais ulivyoandaliwa. ELOG imesema japo visa vya uhalifu vilishuhudiwa maeneo tofauti, IEBC imeendesha zoezi hilo vizuri. Aidha imelalamikia polisi kuwahangaisha waliosusia uchaguzi huo wakiitaka IPOA kuwachukulia hatua wahusika. Katika taraifa, mkuu wa ELOG Regina Opondo, hatua nyingi zinazostahili zilifuatwa kufanikisha uchaguzi huo. Usemi huo ukiungwa mkono na waangalizi wa umoja wa Afrika wanaotaka usalama kudumishwa vilivyo na wakenya kuheshimu uhuru wa IEBC wakati huu.

Show More

Related Articles