HabariMilele FmSwahili

Wenyeji mtaani Kibera walalamika kuhangaishwa na polisi

Wenyeji wa mtaa wa Kibera wanalalamikia kile wanadai kuhangaishwa na polisi. Wanadai idadi ya polisi eneo hilo imekua ikiongezeka kwa kasi tangu jana na kuwa tishio kwao. Wamemetaka insepkta wa polisi Joseph Boinett kuwaondoa polisi hao eneo hilo wakisisitiza wanazingatia amani licha yao kususia uchaguzi. Aidha wanasema hawako tayari kwa zoezi hilo hadi wapewe mwelekeo na kinara wa muungano wao wa NASA Raila Odinga.

Show More

Related Articles