HabariMilele FmSwahili

Watu wawili wauawa kwa kupigwa risasi mjini Bungoma

Watu wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi baada ya  makabiliano kuripotiwa kuzuka baina ya polisi na waandamanaji waliokuwa wamefunga barabara ya Bungoma Mumias Kakamega. Hali ya taharuki imetanda katika eneo hilo huku makabiliano hayo yaliyodumu usiku kucha yakindelea leo. Polisi wanaendelea kushika doria mjini huko kukabili uvunjaji sheria.

Show More

Related Articles