HabariPilipili FmPilipili FM News

Afisa Wa IEBC Aacha Masanduku Ya Kupigia Kura Nje

Maafisa wa polisi eneo la magarini kaunti ya kilifi wanamzuilia afisa mmoja wa IEBC kwa kuacha masanduku ya kupigia kura nje ya kituo cha kuhesabia matokeo.
Mkuu wa polisi eneo hilo Gerald Barasa anasea walimtia mbaroni afisa huyo wa IEBC kwa jina Nicholas Surei aliyekuwa akisimamia zoezi la uchaguzi katika kituo cha Kwa Ndomo huko magarini.
Hii ni baada ya afisa huyo kuwacha vifaa vya uchaguzi nje ya kituo cha kura cha shule ya kiufundi ya mapimo.
Barasa anasema afisa huyo alikuwa hapatikani kwa nambari zake rasmi za simu ya mkononi

Show More

Related Articles