HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana 9 Watiwa Mbaroni likoni

 

Vijana 9 wametiwa mbaroni na maafisa wa polisi eneo la Soweto, likoni hapa mombasa baada ya kumvamia msichana mmoja wakati akielekea kupiga kura.

Inaarifiwa Vijana hao wamemvamia msichana huyo kwa jina la Yvone Mwalesi na kuanza kumpiga wakati akielekea katika kituo cha Vision Soweto huko Likoni kabla ya polisi kuingililia kati na kumuokoa.Kwa sasa 9 hao wanazuiliwa na polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani kwa kosa la kujaribu kumnyima msichana huyo haki yake ya kikatiba.

Onyo Kali limetolewa na Naib Kamishna eneo la Likoni Eric Wamulevi pamoja na OCPD Benjamin Rotich  kwamba yeyote atakaepatikana akivunja Sheria atachukuliwa hatua kali.

 

Show More

Related Articles