HabariMilele FmSwahili

Jaji mkuu David Maraga apiga kura yake katika shule ya Bososi, Nyamira

Jaji mkuu David Maraga amepiga kura yake katika shule ya Bososi kaunti ya Nyamira. Maraga hata hivyo amedinda kuzungumza na wanahabari. Mgobmea urais wa Third way Alliance dkt Ekuru Aukot pia amepiga kura yake katika shule ya wasichana ya Kapedo. Shughuli ya upigaji kura pia inaendelea katika vituo mbalimbali vya upigaji kura kwenye ubalozi wa Kenya katika mataifaya Afrika Mashariki. Kutoka Burundi huko Rwanda na Kampla Uganda idadi ndogo ya wapiga kura pia imejitokeza.

Show More

Related Articles