HabariMilele FmSwahili

ELOG: Asilimia 80 ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wakati

Asilimia 80 ya vituo vya kupiga kura vilifunguliwa kwa wakati, huku asilimia 98 ya vifaa vya uchaguzi vikiwa kwenye vituo hivyo. Haya ni kwa mujibu wa waangalizi wa ELOG wanaosema wameridhishwa na jinis zoezi hilo limeendeshwa maeneo kadhaa nchini. Mwenyekiti Regina Opondo anasema wana imani matokeo ambayo yatatolewa kwenye zoezi la leo yatakuwa huru na wazi. Hata hivyo wameelezea kuwepo visa vya kukatizwa upigaji kura maeneo kadhaa wakitoa wito wa utulivu. ELOG pia imeomba wakenya kutowashambulia waangalizi.kundi hilo litatoa ripoti ya kina baadaye.

Show More

Related Articles