HabariMilele FmSwahili

Mtu mmoja adaiwa kufariki baada ya kupigwa risasi Kondele, Kisumu

Mtu mmoja anadaiwa kufariki baada ya kupigwa risasi akishiriki manadamano na wenzake eneo la Kondele kaunti ya Kisumu. Inadaiwa mwenda zake alikua anawarushia mawe polisi waliokua wanawakabili waandamanaji hao. Idadi ya watu wengine isiojulikana wanapokea matibabu katika hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga.

Show More

Related Articles