
Gavana wa Machakos dkt Alfred Mutua ameusuta upinzani kwa kuwashawishi wafuasi wake kususia kura ya marudio ya urais. Dkt Mutua amemtaja kinara wa NASA kuwa mbinafsi na asiyejali maslahi ya wakenya kwa madai ya kuhujumu uchaguzo hata baada ya kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta mahakamani. Mutua aidha amewapongeza wakazi kaunti hiyo kwa kujitokeza kushiriki zoezi hilo kwa amani.