HabariMilele FmSwahili

Rais Uhuru Kenyatta apiga kura yake Mutomo, Gatundu kusini

Rais  Uhuru Kenyatta  amepiga kura yake eneo la Mutomo Gatundu kusini .Akiongea muda mfupi baada ya kupiga kura yake rais amewataka wananchi kupiga kura kwa amani bila wasiwasi akisema hiyo ni haki ya kila mkenya kikatiba.

Rais Kenyatta amesema demokrasia katika taifa la Kenya imekua kwa kiasi kikubwa akiongeza kuwa maamuzi ya wakenya yanafaa kuheshimiwa kwani kila mtu ana haki ya kupiga ama kutopiga kura.

Show More

Related Articles