HabariPilipili FmPilipili FM News

Naibu Wa Rais Willium Ruto Apiga Kura

Naibu rais William Ruto amefurahishwa na wakenya waliojitokeza kutekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua kiongozi wanayemtaka kuongoza taifa hili.
Akiongea muda mfupi tu baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Sugoi mjini Eldoret, naibu rais amewarai wakenya waheshimu maamuzi ya kila mmoja na kudumisha umoja na mshikamano.
Ruto amesema Kenya ni nchi ya demokrasia na kwamba wale waliosusia uchaguzi pia wana haki kikatiba kufanya hivyo.

Show More

Related Articles