HabariPilipili FmPilipili FM News

Vituo vya kupiga kura Vya funguliwa

Usalama umeimarishwa kote nchini huku wakenya wakitarajiwa kujitokeza kwa wingi kwa uchaguzi wa marudio.Zoezi hilo linatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia saa kumi na mbili asubuhi

Katika baadhi ya maeneo wapiga kura wamefika vituoni kuanzia saa saba usiku ili kupiga kura zao.Wengi wa waliofika vituoni na mapema wanasema wamejitokeza kupiga kura zao ili badae waweze kuendelea na shughuli zao

Kati ya kaunti ambazo wananchi wamejitokeza kwa wingi ni kaunti za nakuru, Eldoret na Uasingishu.kaunti ya kisumu kufikia saa kumi na mbili  vituo vingi vimesalia kufungwa.

Inaarifiwa Maafisa wa tume ya IEBC na hata wapiga kura hakuna aliyefika vituoni kwa ajili ya zoezi hilo.

 

Show More

Related Articles