HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Gavana wa Murang’a aanzisha usafiri bila malipo kwa wenyeji

Baada ya mahakama kuu kutotoa uamuzi wake kuhusiana na kesi ya kuhairisha uchaguzi wa Oktoba 26 wakenya wengi wameibuwa hisia mbalimbali kuhusiana na uamuzi wa mahakama huku ikipelekea wengi wa wakenya kufunga virago kuelekea mashinani wengi wakielekea kupiga kura.

Huku Gavana wa Muranga Mwangi wa Iria akiwalipia wakaazi wa Murang’a nauli ya kuelekea kaunti ya Murang’a ili kupiga kura na wakenya nao walijitokeza kwa wingi.

Idadi kubwa ya wakenya wamesafiri kwa zoezi la upigaji kura hapo kesho huku baadhi wakielekea maeneo ya mashinani kwa kuhofia usalama wao.

Wasafiri kuelekea kaunti ya muranga hata hivyo walinufaika zaidi baada ya serikali ya kaunti hiyo inayoongozwa na Gavana Mwangi wa Iria ikiwalipia wakazi nauli kuhakikisha wanapiga kura hapo kesho.

Show More

Related Articles