Pilipili FmPilipili FM News

IEBC Ya Pata Pigo Mahakamani

Tume ya IEBC kwa mara nyingine imepata pigo mahakamani baada ya mahakama kuu kupuuzilia mbali uteuzi wa maafisa 291 wa kusimamia uchaguzi katika maeneo mbalimbali nchini.
Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama kuu George Odunga.
Katika uamuzi wake Odunga amesema tume ya IEBC ilikiuka sheria wakati wa kuwateua maafisa hao.
Akiongea nje ya mahakama ya juu jijini Nairobi wakili wa NASA James Orengo anasema kufuatia uamuzi huo wa mahakama itakuwa kinyume cha sheria kuendelea na uchaguzi hapo kesho.

Show More

Related Articles