HabariMilele FmSwahili

Uchaguzi wa urais utaandaliwa kesho kama ulivyoratibiwa

Uchaguzi wa urais utaandaliwa kesho ulivyoratibiwa. Hii ni licha ya uamzi wa mahakama ya juu kutaja uteuzi wa maafisa watakaosimamia uchaguzi huo maeneo bunge kuwa si halali. Tume ya IEBC katika taarifa imesema uamzi huo haukuwazuia maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwani haukufutilia mbali tangazo katika gazeti la serikali lililochapisha majina yao. Awali jaji George Odunga alisema IEBC haikufuata sheria katika kuwateua maafisa hao. Hata hivyo wakili wa nasa James Orengo anasema hawatautambua uchaguzi huo kwa madai mahakama imetaja wasimamizi wake kutokua halali.

Show More

Related Articles