HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Polisi wamevamia makaazi ya Khalwale , Kakamega

Polisi hii leo wamevamia makazi ya aliyekuwa seneta wa Kakamega Boniface Khalwale katika eneo la Ikolomani kaunti ya Kakamega wakidai kutafuta vifaa anavyodaiwa kuwa navyo ili kuzua rabsha wakati wa uchaguzi wa marudio Alhamisi hii.

Wakiongozwa na afisa mkuu wa upelelezi katika kaunti ya Kakamega bernstein shari maafisa hao walifika na agizo la mahakama lakini hawakufaulu kupekua makazi hayo kwa kuwa agizo hilo halikuwa na kipengee cha kiusalama.

Show More

Related Articles