HabariMilele FmSwahili

Shehena ya mwisho ya karatasi za kupigia kura kuwasili nchini leo jioni

Shehena ya mwisho ya karatasi za kura itawasili nchini baadaye leo jioni. Tume ya uchaguzi IEBC imedhibitisha kuwa shehena hiyo ya karatasi 116 zitakazotumika katika kaunti 14 itawasilishwa saa 12 jioni kutoka Dubai. Wakati uo huo kampuni ya Ot Morho imesema imefanyia ukaguzi mfumo yake ya kupeperusha matokeo ya uchaguzi na kubaini iko salama. Kampuni hiyo imeelezea kuwa inashirikiana na IEBC kuhakikisha kura ya Oktoba 26 haitakumbwa na hitilafu zozote.

Show More

Related Articles