HabariMilele FmSwahili

Moto wateketeza darasa moja na ofisi katika shule ya msingi ya Shivakala

Watu wawili wanauguza majeraha katika hospitali ya rufaa ya Kakamega  kufuatia mkasa wa moto ulioteketeza darasa moja na ofisi kwenye shule ya msingi ya Shivakala kata ya Bukhungu eneo bunge la Lurambi. Wakazi wa sehemu hiyo wanadai kuwa huenda moto huo uliwashwa kimaksudi na mtu aliyetumia petroli usiku wa kuamkia leo. Viongozi kutoka eneo hilo wakiongozwa na mbunge Titus Khamala wamefika katika shule hiyo na kuahidi kutoa msaada wa ujenzi wa majengo  hayo upya.

Show More

Related Articles