MichezoMilele FmSwahili

Ronaldo atuzwa mchezaji bora duniani

Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandada ,hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo.Ronaldo aliwapiku fowadi wa Barcelona Lionel Messi na Neymar anayetokea Paris Saint Germain.
Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki mwaka huu, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na ligi ya mabingwa Ulaya Champions League.
Tuzo hiyo kwa mchezaji bora wa kike  ilinyakuliwa na  mchezaji wa Uholanzi Lieke Martens, anayeichezea Barcelona.
Aliwahi pia kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi iliposhinda mashindano ya Euro 2017.

Show More

Related Articles