HabariPilipili FM News

Tobiko Agiza Fred Outa na Ruth Odinga Wakamatwe

Mkurugenzi wa mashitaka ya umma Keriako Tobiko ameagiza seneta wa Kisumu Fred Outa pamoja na aliyekuwa naibu gavana wa Kisumu Ruth Odinga wakamatwe na kufunguliwa mashtaka.

Hii ni baada ya wawili hao kuvuruga  mikutano ya mafunzo ya maafisa wa IEBC katika kaunti ya kisumu wiki iliyopita.

Katika barua yake, Tobiko amemwagiza mkurugenzi wa jinai Ndegwa Muhoro kuwafungulia mashitaka wawili hao kwa tuhuma za kuingilia mkutano wa IEBC bila idhini, na kuchochea umma , ikiwemo  kuhusika katika uharibiifu wa mali ya tume hiyo

Show More

Related Articles