HabariPilipili FM News

Shehena ya Pili Ya Karatasi za Uchaguzi Ya Tarajiwa Kuingia Nchini Leo.

Awamu ya pili ya makaratasi ya kura za marudio inatarajiwa kuingia nchini  saa kumi na moja jioni  hii leo katika uwanja wa ndenge wa Jomo Kenyatta.

Tume ya IEBC kupitia mtandao wake wa twitter  imesema makaratasi hayo yatatumika katika kaunti 22, huku makaratasi mengine yakitarajiwa kuingia nchini tarehe 23 Octoba saa kumi na moja jioni.

Awali siku ya jumamosi ndege lililokua likibeba tani 16 za makaratasi hayo iliingia  nchini  ikibeba makaratasi ya kura yatakayotumika katika kaunti za Marsabit, Turkana ,Mandera, Wajir, Tana river ,Lamu, Garissa, Isiolo, Samburu, Laikipia na maeneo ya nje ya nchi.

Naibu wa kamishna wa tume hiyo, Consolata Nkatha amewahakikishia wakenya kuwa tume hiyo iko tayari  kufanikisha uchaguzi wa marudio licha ya changamoto zilizowakumba kwenye uchaguzi wa agosti 8.

Show More

Related Articles