HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Kuskiza Kesi Zakupinga Uchaguzi Leo.

Huku tume ya IEBC ikimalizia mandalizi ya uchaguzi wa marudio unaopangwa kufanyika siku ya alhamisi, mahakama kuu leo inatazamiwa kusikiza kesi mbili zinazolenga kusitisha zoezi hilo.

Moja kati ya kesi hizo iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge wa Kilome Harun Mwau ambaye anataka uchaguzi wa marudio usimamishwe, kwa msingi kuwa tume huru ya uchaguzi nchini IEBC imeshindwa kuafikia vigezo vya katiba .

Mwau anasema kulingana na uamuzi  uliotolewa na mahakama ya upeo wakati wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa agosti 8,ulihitaji IEBC kuteua wagombea wote upya kutoka kwa teuzi za vyama.

Naye Okiya Omtatah ambaye amewasilisha kesi nyingine katika mahakama kuu anasema hakuna mazingira mazuri ya kuandaa kura za marudio siku ya alhamisi.

Omtata anaitaka mahakama kutoa mwelekeo wa kuongoza serikali baada ya oktoba 26, kutokana na kile anasema huenda kukawa na gogoro wa kisiasa hasa iwapo uchaguzi hautafanyika kwa mda wa siku 60 uliotolewa na mahakama.

Show More

Related Articles