HabariPilipili FmPilipili FM News

Dori Alaumu Polisi Msambweni.

Mbunge wa Msambweni  Suleiman Dori amekashifu maafisa wa polisi huko Diani kaunti ya Kwale  kwa kile amekitaja kama kuwahangaisha na kuwachapa wakaazi wa eneo  hilo , wakati wa oparesheni ya kusaka bunduki wanazodai zinamilikiwa na Wananchi kinyume na sheria.

Dori ameshinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu wa polisi huko msmbweni Joseph chebusit aliyemtaja kutokuwa na uhusiano Bora na Wananchi.

Kwa upande wake muwakilishi wa Kinamama Zulekha Hassan amezitaka idara za usalama  kuendeleza oparesheni zao kwa njia ya nidhamu na kuwa na ushirikiano mzuri na wananchi.

Kwa upande wake kamanda wa polisi kaunti ya kwale Kenneth Kimani amewataka wakaazi kudumisha amani na usalama, huku akitoa hakikisho la kuwaachilia huru zaidi ya vijana 30 waliokuwa wamezuiliwa katika kituo cha polisi  Cha Diani baada ya kukamatwa na polisi katika operesheni hiyo.

 

Show More

Related Articles