HabariMilele FmSwahili

Kenya kuadhimisha sherehe ya Mashujaa leo katika bustani ya Uhuru

Kenya leo inaadhimisha siku ya mashujaa, shereha za maadhimisho hayo zikitarajiwa kuandaliwa katika bustani ya Uhuru hapa Nairobi. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa hotuba kutoka kwake. Hotuba ya rais Kenyatta inatarajiwa kuangazia maswala mengi muhimu yanayokabili taifa. Kufutia sherehe hii, usalama umedumishwa vilivyo katika bustani ya Uhuru ambako maadhimisho hayo yataandaliwa. Polisi wanasema wamezidisha doria kuzuia visa vyovyote vya ukiukaji sheria. Mshirikishi kanda ya Nairobi Bernard Leparmarai anasema polisi watakuwa pia wakishika doria katikati mwa jiji kupambana na uhalifu wowote.

Show More

Related Articles