HabariMilele FmSwahili

Kimani Ngunjiri: Mgogoro wa siasa watishia uchumi wa nchi

Wabunge wa Jubilee wameelezea haja ya kutatuliwa mgogoro wa kisiasa nchini wakionya unatishia kuyumbisha uchumi wa taifa. Kulingana na mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri hali ya kisiasa nchini imepelekea hazina kuu kutotoa kwa wakati fedha za maendeleo kwa serikali za kaunti hali iliyokwamisha utekelezaji miradi hiyo. Ngunjiri ametaka wadau wote kupata mwafaka upesi ili kuwaepushia wakenya mahangaiko zaidi. Kauli sawa imetolewa na mbunge maalum Dkt David Ole Sankok.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.