MichezoMilele FmSwahili

Harambee Stars kuchuana na Iraq kwenye mechi ya kirafiki leo

Timu ya taifa Harambee Stars hii leo itashuka ugani dhidi ya wenyeji Iraq kwenye ngarambe ya kirafiki katika uga wa kitaifa wa basra.

Kikosi hicho kimepigwa jeki na kuwepo kwa wachezaji wanaosakata mataifa ya nje akiwemo Michael Olunga wa kule Uhispania, Eric Marcelo Ouma na Abud Omar wote kutoka Georgia, Anthony akumu, Jesse Were na David Calabar wote kutoka Zesco United kule Zambia, Clifftone Miheso na John Mark Makwatta kutoka Buildcon.

Hata hivyo okumbi anasema kwamba huenda Marcelo asishiriki mchuano wa leo kufuatia jeraha na Masud Juma bado anachunguzwa kubaini iwapo atasakata.

Mtanange huo dhidi ya Iraq unang’oa nanga saa moja kamili jioni.  Siku ya jumapili stars wana kibarua kingine dhidi ya Thailand.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker